Image
Image

TANZIA:Aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe afariki dunia jijini Dar es Salaam.

Aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Mohamed Abood amesema kuwa bado haijafahamika kilichosababisha kifo chake mara moja, isipokuwa huenda ikawa kimesababishwa na maradhi yatokanayo na umri.
"Ni ngumu kusema sababu za kifo lakini pengine ni uzee, maana umri wake ulikuwa umekwenda"amesema Abood.
Amesema taarifa rasmi ya serikali itatolewa baadaye na kuwataka wazanzibar wakiwemo ndugu jamaa na viongozi mbalimbai kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Aidha Maziko yatafanyika kesho visiwani Zanziabr baada ya mwili wake kusafirishwa kutoka Dar es salaam, leo.
                                                Historia
Aboud Jumbe Mwinyi alizaliwa Tarehe 14 mwezi Juni mwaka 1920, na amefariki leo tarehe 14 Agosti mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 96.
Wakati wa uhai wake alishika nyazifa mbalimbali ikiwemo ya urais wa awamu ya pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar.
Alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia April 11 mwaka 1972 hadi tarehe 30 Januari mwaka 1984 akichukua nafasi ya Rais wa Kwanza wa nchi hiyo Abeid Karume aliyeuawa April 7, 1972.
Alishika nafasi hiyo ya urais kwa kuhaguliwa na Baraza la Mapinduzi wakati huo likiwa chini ya chama cha ASP kabla hakijaungana na TANU na kuzaa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.
Mwaka 1979, Jumbe alisukuma mabadiliko ya Katiba yaliyotenganisha majukumu kati ya Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi.
Mabadiliko mengine yaliyofanyika katika katiba ni kuwezesha wananchi kumchagua Rais kupitia uchaguzi wa kidemokrasia badala ya utaratibu uliokuwepo ambapo Rais alikuwa akichaguliwa na Baraza la Mapinduzi.
Jumbe atakumbukwa kwa kuwa kiongozi mwenye msimamo thabiti katika kusimamia maamuzi yake na serikali, wakati wa uhai wake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment