TOFAUTI na matunda mengine, ndizi zinafaida kubwa katika mwili wa
binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya
aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalshiamu, wanga, fosiforas,
madini ya chuma, vitamin A,B,C na maji.
Ndizi zina uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi zaidi, tena zina nishati, sukari iliyomo ndani yake ni chanzo kizuri cha nishati.
Husaidia kuondoa chunusi. Kwa kuchanganya ndizi mbivu, maziwa na asali
na kuzisaga ili kupata urojo ambao utatumia kupaka kwenye maeneo
yaliyoathirika, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.
Fanya hivyo kila siku na hakikisha unakaa na mchanganyiko huo kwa
muda usiopungua dakika 30 hadi 40, kisha osha na maji ya baridi
ikiwezekana yaliyopozwa na jokofu.
Ndizi katika ‘diet’ zina nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza
uzito, hivyo unaweza kutumia ikiwa unahitaji kupunguza ama kuongeza
uzito wako.
Kwa wajawazito ni chakula kizuri mno, kwani kina kiwango kikubwa cha
‘folic acid’ ambayo inaweza kufyonzwa kwa urahisi na kiumbe kilicho
tumboni. Ikiwa mjamzito atatumia ndizi mara kwa mara ni wazi kuwa
atakuwa mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia.
Pia ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo na kukosa choo.
Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina
hakika kama watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo
linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na
150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.
Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika
kubadili mtizamo wako na kuziangalia ndizi kama tunda muhimu katika
kuupa nguvu na kuulinda mwili wako dhidi ya maradhi hatari ambayo hayana
tiba.
Wanamichezo pia wanapaswa kuliona tunda hili kuwa ni muhimu katika kuipa miili yao nguvu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment