Mwanariadha
wa Jamaica, Usain Bolt, ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa
kwanza kushinda nishani ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika
mbio za mita mia moja, kwenye michezo ya olimpiki ya Rio 2016.
Bolt,
29, amechukua muda wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika
michezo ya olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya
olimpiki mjini Beijing 2008, na London 2012.
Gatlin, ambaye amepigwa
marufuku mara mbili kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli, alimaliza
sekunde 0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.
"Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda," Bolt ameiambia BBC.
Mwanariadha
wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha
muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica
Yohan Blake.
Bolt anatazamia kuondoka Rio na nishani zaidi za dhahabu
katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi ilivyokuwa
katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.
Mwanariadha huyo
anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa
atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa
dunia mwaka 2017.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)










0 comments:
Post a Comment