Kufuatia vyombo vya habari mbalimbali nchini kutoa habari ambayo
inamhusu Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi kuwa
anatakiwa kufika mahakamani Agosti, 24 mwaka huu kujieleza kwanini
asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa Dola 598,750 (Bil.
1.20), wakili wa Dk. Mengi, Deogratias Ringia amekanusha habari hiyo.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na wakili Ringia, amesema kuwa akiulizwa na
watu mbalimbali kama ni kweli kuna hati imetolewa na Mahakama Kuu
ikimtaka mteja wake Dk. Mengi kufika mahakamani kujieleza kwanini
asifungwe baada ya vyombo mbalimbali kuripoti kuwa anatakiwa kufika
mahakamani lakini jambo hilo halina ukweli.
"Mhusika
mkuu katika kesi hiyo ni kampuni Inayoitwa KM Prospecting Limited
ambayo Dk. Mengi siyo mwanahisa wala mkurugenzi katika kampuni hiyo.
Kampuni hiyo ndiyo iliingia kwenye mkataba na wadai iliyopelekea kesi
hiyo ya madai," alisema Ringia.
Ringia
alisema hatua ya kumuunganisha Dk. Mengi katika kesi hiyo lilikuja
baada ya mahakama kuamua hoja mbili zinazohusu kesi hiyo ndipo wadai
ambao ni wafanyabiashara Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles
Mgweo kumuingiza Dk. Mengi katika kesi licha ya kuwa hausiki.
Baadhi
ya vyombo vya habari vilivyoandika habari hiyo ni pamoja na gazeti la
Jambo Leo, Daily News, The Citizen na mtandao wa Habari Leo Online.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment