Pia
ameitaka Wizara hiyo kupitia upya sekta ya ushirika kwa kuanza na
viongozi walipo ndani ya wizara hadi mikoani kuhakikisha kama wanafanya
kazi zao ipasavyo na kuwaondoa watakaobainika kwa uzembe.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo leo (Jumatatu, Agosti 08, 2016) wakati akifunga
maadhimisho ya sherehe za nane nane kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
yaliyofanyika kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema mkulima,
mfugaji na mvuvi mdogo au mmoja mmoja hawezi kupunguza umaskini bila ya
kuwa na chombo cha kuwaunganisha na kuwapa nguvu ya kutetea bei ya
mazao yao kama ushirika. Aidha, ushirika imara utawasaidia kutafuta
soko, kupata mikopo ya riba nafuu.
Amesema
pamoja na umuhimu wa kuwepo kwa ushirika, tasnia hiyo imewaumiza
wakulima wengi na kuwafanya kukata tamaa katika uzalishaji kutokana na
usimamizi mbovu, ubadhirifu na ubabe wa baadhi ya viongozi wa ushirika.
“Wahimizeni na kuwashawishi wakulima, wafugaji na wavuvi kujiunga katika
vikundi vya ushirika vya uzalishaji na SACCOS. Aidha, elimu ya ushirika
inayotolewa kwenye maonesho ya mwaka huu, iwe changamoto kwenu kwamba
umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,” amesema.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali
haitamvumilia mfugaji anayelisha katika maeneo ya hifadhi na vyanzo vya
maji, Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kulinda maeneo hayo.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha
alisema sekta ya kilimo imekuwa na mafanikio makubwa ambapo katika
kipindi cha miaka mine mfululizo nchi imeweza kuzalisha chakula cha
ziada, ambapo kwa mwaka huu imezalisha kwa asilimia 123.
“Mafanikio
hayo yanachangiwa jitihada za Serikali katika kutoa ruzuku ya pembejeo,
taasisi za utafiti ambazo zimekuwa zikitafiti aina bora ya mbegu
zikitafuta mbegu bora na wakulima walioamua kuwekeza kwenye kilimo,”
alisema.
Naibu
Waziri Ole Nasha alisema katika ukanda wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) ni nchi mbili tu za Tanzania na Zambia kati ya
nchi 15 za jumuia hiyo hazikabiliwiu na baa la njaa.
Licha
ya mafanikio hayo Naibu Waziri huyo aliwaomba wakulima kuendelea
kuzalisha kwa kufuata kanuni bora za kilimo pamoja na kutumia pembejeo
bora.
Naye
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini, Ladislaus Mwanakatwe ameipongeza Serikali kwa
jitihada zake za kuwatetea pamoja na utatuzi wa kero za muda mrefu
zilizokuwa zinawakabili wakulima ikiwemo ya tozo.
Hata
hivyo Mwanakatwe ameiomba serikali kuitafutia ufumbuzi changamoto ya
upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo. Pia ameomba
Serikali iwezeshe Benki ya Kilimo (TADB) kufungua matawi katika mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini ili wakulima wake waweze kupata mikopo kwa
urahisi.
0 comments:
Post a Comment