Image
Image

Zaidi ya Shilingi bilioni tatu zatumika kulipa mikopo kwa wanafunzi hewa jijini Dar es Salaam

Na.Avila Kakingo,na Festo Milia Dar es Salaam.
Zaidi ya Shilingi bilioni tatu zatumika kulipa mikopo kwa wanafunzi hewa 2192 wa vyuo vikuu 31 vilivyofanyiwa uhakiki nchini huku serikali ikitoa siku 7 kurejesha fedha za wanafunzi ambao hawapo shuleniHayo yamesemwa na Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa vyuo hivyo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usaili, matokeo ya majaribio na matokeo ya mitihani pamoja na namba za akaunti za benki ambapo  mikopo hulipwa huko.
Profesa Joyce amaesema kuwa vyuo vikuu vinatakiwa kuwasilisha taarifa zote za kitaaluma na za kibenki za wanafunzi kwa wakati ili kuiwezesha bodi ya mikopo kufanya marekemisho ya stahiki katika kumbukumbu zao ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Pia amesema kuwa hatu kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wote watakaohusika kufanikisha malipo kwa wanafunzi ambao hawapo vyuoni.
Profesa Joyce amesema kuwa uchunguzi zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambazo zimelipwa kwa watu wasiostahili.
Pia wakuu wa vyuo(VCs Principals) wametakiwa kuweka mfumo wa sahihi uhakiki wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa bodi ya Mikopo na wakuu hao watawajibika kwa usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki limebaidi kuwa na udanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi kwa kuwa kunawanafunzi ambao hawakfanya mitihani na wengine wamefeli lakini wameandikiwa PASS ili waendelee kupata mkopo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment