Mwezi
mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni Ukuta kupinga inachokiita
ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia, leo
inatarajia kutoa mwelekeo wa mkakati huo.
Operesheni hiyo ilipangwa
kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara
kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na
vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa
kufanya mikutano ya hadhara.
Siku moja kabla ya kufanyika kwa
operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza
kuisitisha kwa mwezi hadi kesho, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini
kusemezana na Rais John Magufuli na Serikali yake.
Jana, Mwanasheria
Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema: “Kuhusu Ukuta, kesho (leo) tutatoa
msimamo wetu juu ya kitu tutakachofanya.”
Alisema operesheni hiyo
ilisitishwa kutokana na sababu za msingi zilizoelezwa, hivyo kauli ya
chama hicho leo itafafanua kwa kina kuhusu mambo yote yaliyojitokeza
katika kipindi hicho cha mwezi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA, Tumain Makene alipost taarifa hii katika ukurasa wake.
Wakati viongozi hao wakieleza hayo, hadi jana hakukuwa na taarifa zozote za kufanyika kwa kikao kati ya viongozi wa dini na Serikali.
Viongozi hao waliitaka Serikali na Chadema kufikiria amani ya nchi na kutafuta njia mwafaka za kumaliza msuguano wa kisiasa hasa baada ya chama hicho kushikilia msimamo wake wa kufanya mikutano na maandamano.
Wakati Chadema wakijipanga kutoa tamko lao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alisisitiza kuwa Oktoba mosi ni Siku ya Kupanda Miti jijini humo ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment