Image
Image

LIPUMBA afunguka*Amshukia Maalim na mkakati wa kuiua CUF Bara na Amlipua Lowassa.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Haruna Lipumba akjizungumzia sakata lake la kuvuliwa uanachama wakati wa mazungumzo maalumu na CLOUDS FM amesema mpaka maamuzi hayo yanafanywa kwanza hakuwa na barua ya kusimamishwa uanachama mpaka waliposikia kuwa atakuwa na mazungumzo na Clouds ndipo wakamletea barua ya kumsimamisha.
Amesema Barua ilikuwa ya tarehe 30 Agosti, 2016 na aliipata jana tarehe 7 Septemba.
Azungumzia sababu za kutomkubali Lowassa.


"Sababu za msingi za kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA, ni
kwamba ukiwa katika siasa unahitaji uongozwe na misingi na 'principals'
na hoja kwamba mnagombea kitu gani, na sisi tulianzisha UKAWA kwa kusema
kwamba tutafute nchi, serikali na dola inayowajibika ambayo
inatengeneza mambo vizuri, inatumia rasilimali vizuri itapambana na
ufisadi na itajenga demokrasia ya kweli katika nchi yetu, ukiwa na
misingi hiyo kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo
na tulikuwa wote kwenye bunge la katiba na Mh. Edward Lowassa alikuwepo
kwenye bunge hilo hakuwa mmoja ya wabunge aliyeunga mkono rasimu ya
Katiba" Ibrahim Lipumba #Live #PowerBreakFas akizungumza kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu kuwa mwenyekiti wa CUF mwaka jana.
"Kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha
kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na ukumbuke
Mh. Edward Lowassa alikuwepo katika bunge la katiba ya rasimu ya Jaji
Warioba na hakuunga mkono rasimu hiyo kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa
na ile misingi iliyotuunganisha na kuanzisha UKAWA kuja kumchukua Edward
Lowassa ndiye awe mgombea urais wa watu wanaounga mkono rasimu ya Jaji
Warioba" Ibrahim Lipumba #Live #PowerBreakFast akizungumza kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu kuwa mwenyekiti wa CUF mwaka jana.
Amzungumzia Maalim Seif.
#PowerBreakfast "Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.
Wanasema nahujumu chama, lakini tuna wabunge 10, bado wanataka kuwafukuza wengine, hapo nani anahujumu" - Prof. Lipumba.
Azungumzia hatua za kuvuliwa uanachama.
- Mbunge wa Kaliua Mh. Sakaya bado ni mwanachama na Mbunge, kikao kilichofanyika kumsimamisha uanachama hakina uhalali, Mh. Sakaya ilibidi awe kwenye Kikao hicho kama Naibu katibu Mkuu Bara ambaye ni msaidizi wa Katibu mkuu ndio alikuwa anahusika kuandaa kikao lakini hakuwa na taarifa mpaka siku moja kabla ya kikao ndio akajulishwa.
- Vikao vya CUF vina utaratibu, hiki hakikufuata utaratibu maana cha kimafia.
- Vyama vinavyounda UKAWA vilikubaliana kumsimamisha Mgombea mmoja kati ya Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Dr. Kahangwa wa NCCR Mageuzi.
- Nilikaa kikao na Dr. Slaa na Dr. Kahangwa nyumbani kwangu na tukakubaliana kwakuwa wenzetu CHADEMA wamejiandaa na wana uwezo mkubwa basi wamsimamishe Mgombea wa Urais (Dr. Slaa), CUF hatukuwa na uwezo.
Mkakati wa Mbowe na Seif kumshawishi lowassa kujiunga UKAWA.


- Wakati tunapanga kumbe Mbowe na Seif walikuwa wanamshawishi Lowassa ahamie CHADEMA na awe mgombea Urais.Mh Mbowe na Maalim walikuwa wanawasiliana peke yao katika kuhakikisha EL anakuwa mgombea kwa bendera ya UKAWA bila kushirikisha kamati tendaji za vyama vyao.
- Tulikuwa tumekubaliana kutosimamisha mgombea wa makapi, tulitaka mgombea aliyetoka ukawa aliyekuwa anaunga mkono rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, Lowassa hakuwa anaunga katiba ya Jaji Warioba.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment