WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Joyce Ndalichako ameitaka Bodi mpya ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
(TCU), aliyoizindua Dar es Salaam jana, kushughulikia kwa ukamilifu
changamoto ndani ya tume hiyo.
Profesa Ndalichako alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa
wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na vyuo wanavyosoma, jambo ambalo
anaamini kama likifanyiwa kazi vizuri malalamiko yatakwisha.
“Tunaelewa wanafunzi ni watu wa kulalamika kila wakati, yapo malalamiko ambayo yana tija lazima yatatuliwe.
“Kwa mfano malalamiko yanayohusu uvurugaji wa matokeo au taratibu zinazowakandamiza kutoka kwa walimu wa vyuo vikuu,”alisema.
Akitoa mfano wa taratibu kandamizi katika vyuo hivyo, Profesa
Ndalichako alisema mwanafunzi anapopoteza kitabu cha chuo hulipishwa
mara tatu ya gharama huku akiwa ni mtoto wa masikini, hali
inayosababisha washindwe kuazima vitabu wakihofia kulipishwa gharama
kubwa.
Alisema kuna baadhi ya vyuo vimekuwa vikiwataka walimu kutoa taarifa ya kuacha kazi miezi mitano kabla ya kuacha kazi.
Waziri alisema sheria mama inamtaka mwajiriwa kutoa taarifa ya kuacha kazi kwa mwajiri miezi mitatu kabla ya kuacha kazi.
Pia alisema amepokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Ifakara mkoani Morogoro, Mei mwaka huu juu ya walimu wa chuo hicho
kuvuruga matokeo yao.
Aliitaka TCU kufanya utafiti wa wanafunzi walioko vyuoni kubaini
wanafunzi wasio na sifa kutokana na baadhi ya vyuo kuingiza wanafunzi
kinyemela bila kupitia TCU au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE).
Bodi hiyo itakayodumu kazi kwa miaka mitatu inaongozwa na Mwenyekiti, Profesa Philip Mtabaji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment