Image
Image

Ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL yawasili JNIA ikitokea Canada.

Hatimaye ndege moja wapo ya zile mbili zilizonunuliwa na Serikali ya awamu ya tano inatarajiwa kutua leo saa saba (1015 UTC) ktk uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA),safari ya ndege hiyo kuja nchini ilianza mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia na kutoka Ethiopia itatua Dsm ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada
Ili kuepusha muingiliano na ndege nyingine za abiria (scheduled flights) za ndani ya nchi na zile za kimataifa katika eneo la Terminal Two,ambapo mida hiyo itakuwa ndio "peak hours",ndege hiyo itakapotua itaongoza moja kwa moja eneo la Terminal One,VIP Apron kwa ajili ya kupokelewa na viongozi mbalimbali wa kiserikali.
Kama ilivyo utaratibu na utamaduni wa usafiri wa anga..kabla ya kuingia "apron" ndege hiyo itapata "Water Cannon Salutation" kutoka Magari ya Jeshi la Zimamoto kama ishara ya kuikaribisha kabla ya kuvuka gate kuingia eneo la maegesho.Na baade kutakuwa na hatua za kukata utepe,hotuba na mengineyo.
Wakati ndege hii ikiingia leo,ndege ya pili ambayo tayari imekaguliwa na Maafisa wa Ukaguzi toka Mamlaka ya Anga Tanzania(TCAA),itakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania 22/09/2016 na kuanza safari ya kuja Tanzania 23/09/2016.
Wakati huo huo tuendelee kufahamu undani wa ndege hizi:
BOMBARDIER DASH8 Q400
Jamii Yake Nyingine: Bombardier Dash 7/8 & Q 200/300/400.
Kutengenezwa: CANADA
SIFA
Abiria: (passengers) 74-90
Urefu: (Length) 32.6 mita.
Kimo: (Height) 6.40 futi.
Upana: (Width) 8 futi.
Nguvu/Injini: (HorsePower)10,142 HP
Spidi: (AirSpeed) 666.7 Km/h
Umbali Inayoenda: (Max.Range) 2522.4 km.
Umbali Kuruka Juu: (Cruising Altitude) 27,000 futi.
Uzito Wa Kubeba: (Max Payload) 8.7 tani.
Full Tank: (Fuel Capacity) 6617 lita.
Mda Inayotumia Kufika Umbali wa Juu: (Time to Cruising Altitude)18 dak.
Urefu Njia ya kurukia: 1067mita
Urefu Njia ya Kutua : 1286mita Ulaji Mafuta: (Fuel Economy/Km) 16,940/-Tzs kila 1.8 km.
Bei kwa Ndege Moja: (Price range)
66 bilioni.
These features are between Min & Max. Visualization
Jf be the first to know....Habari zitakujia moja kwa moja!!
===================================================================
Hatimaye mdege moja kati ya mbili mali ya ATCL imetua ktk ardhi ya Tanzania.Ndege hiyo yenye Test Reg # C-FIFG imetua JNIA kati ya majira ya saa 0914 UTC(1214 Local) na kupokelewa na maafisa kadhaa wa Serikali.
Mara baada ya kutua,ndege hiyo imepelekwa moja kwa moja eneo la maegesho la Jeshi la Wananchi Tz(JWTZ-AIRWING HANGAR) ambapo itakaa mpaka ile ya pili ifike na hivyo Serikali kukabidhiwa rasmi.

Source:JF.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment