Ofisi
ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya
jamii kwamba Makamu wa Rais, SAMIA SULUHU HASSAN ameomba kujiuzulu
nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni uongo na uzushi na ukweli wowote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais, taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka taifa kwenye taharuki.
Imesema
Makamu wa Rais yupo bega kwa bega na Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI
katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchiili kuwaletea
wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi
kupuuza taarif hiyo ambayo inaleng kupotosha umma kuhusu ushirikiano
mzuri uliopo baina ya viongozi wa taifa.
Ofisi ya Makamu wa Rais
inawahimiza Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo
vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment