OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imebainisha kuwa katika kipindi cha
robo ya pili ya mwaka huu, pato la taifa limeendelea kukua kwa kasi ya
asilimia 7.9 ikilinganishwa na asilimia 5.8 ya robo ya pili ya mwaka
jana.
Aidha, imetaja sekta zilizochangia kukua kwa kasi kwa pato hilo kuwa
ni kilimo, viwanda,uchukuzi, ujenzi, madini na umeme kupitia gesi
asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu taarifa hiyo
ya uchumi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa
NBS Dk Albina Chuwa, alisema kutokana na kasi ya uchumi inavyokwenda kwa
sasa, huenda ifikapo Desemba mwaka huu, kwenye taarifa ya robo ya tatu
ya mwaka, pato hilo likaongezeka zaidi.
Alisema kwa mujibu wa takwimu zilizopo pato hilo la taifa limefikia
jumla ya thamani ya Sh trilioni 11. 7 ikilinganishwa na Sh trilioni 10.9
katika kipindi kama hicho cha mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment