WANAFUNZI 3,918 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano
awamu ya pili kujaza nafasi zilizokuwa wazi kutokana na ufinyu wa nafasi
na baadhi ya wanafunzi kutoripoti kwa wakati.
Taarifa
iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe ilisema kati ya wanafunzi hao
wasichana ni 2,413 na wavulana 1,505.
“Kuchaguliwa
kwa wanafunzi hao kumefuatia kuwapo kwa nafasi zilizoachwa wazi na
wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni tangu kuchaguliwa kujiunga na
kidato cha Tano katika awamu ya kwanza” alisema Mhandisi Iyombe.
Aidha
Mhandisi Iyombe alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 1,864 sawa na
asilimia 47.58 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati
ambapo kati yao wasichana 1,099 na wavulana 765.
Mhandisi
Iyombe aliongeza kuwa katika masomo ya Sanaa na Biashara wanafunzi
takribani 2,054 (52.42%) wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo, ambapo
kati yao wasichana ni 1,314 na wavulana 740.
“Wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016
wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo
mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya
tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii” alisema Mhandisi Iyombe.Majina
ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili
mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ambayo
ni www.tamisemi.go.tz.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment