Tanzania
imesema haina mpango wa kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
(ICC) iliyoko The Hage nchini Uholanzi licha ya kwamba baadhi ya nchi
barani Afrika zimeonesha nia ya kujitoa na kutokua na imani na utendaji
kazi wa mahakama hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt.
Augustine Mahiga wakati akizungumza na East Africa Radio kuhusu msimamo
wa Tanzania katika mahakama hiyo.
Amesema mpaka sasa hakuna sababu ya
kujiondoa katika mahakama hiyo kwakuwa nchi haijafika mahali ambapo
kuna watu au vikundi vya watu ambao wamehusika na makosa ya jinai,
makosa ya kimbari, makosa dhidi ya binadamu au makosa ya kivita,hivyo
Tanzania inaendelea kutafuta suluhu kwa kuona kama mahakama hiyo inaweza
kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya sheria zake ili kuhimarisha
utendaji wa haki na uwazi wa mahakama hiyo.
Amesema Tanzania
haijaombwa kuunga mkono swala la kujitoa katika mahakama hiyo kwakuwa
kulikuwa na mjadala wa nchi za Umoja wa Afrika zijiondoe kwa pamoja
katika mahakama hiyo kwa umoja lakini hakukuwa na makubaliano wala
muafaka wa jambo hilo hivyo hakuna sababu ya kujitoa katika mahakam
hiyo.
Chanzo: ITV
Home
News
Slider
Dkt.Mahiga:Tanzania haina mpango wa kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment