Siku
moja baada ya kuwepo tofauti kati ya mkuu wa mkoa wa Arusha na Mbunge
wa Arusha Mjini Godbless Lema kuhusu mradi wa ujenzi wa hospitali
itakayotoa huduma kwa mama na mtoto mkoani humo na 19 Octoba 2016
kuonekana taarifa zinazodai kuwa Rais Magufuli katengua uteuzi wa Mkuu
wa Mkoa Mrisho Gambo zimebainika sizakweli.
Taarifa kamili kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa Rais Dkt John Pombe
Magufuli amempigia simu na kumwambia kuwa ana imani naye na kuwa
hajafikiria kutengua uteuzi wake labda kumpandisha cheo.
Hayo
yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari baada ya taarifa kuhusu Rais
kutengua uteuzi wake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Mkuu wa
mkoa alisema kuwa alipigiwa simu nyingi na watu wengi lakini kabla
hajawajibu Rais Magufuli akampigia simu na kumueleza kuwa ana imani naye
na kuwa ahakikishe anawatumikia wananchi wa Arusha kwani yeye sio bosi
wao bali ni mtumishi wao.
Pia mkuu wa mkoa alieleza kuwa Rais amempa
maagizo ya kuhakikisha anasimamia wananchi wa mkoa wa Arusha walipe kodi
kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na nchi kwa ujumla.
Aidha, ili
kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli ndiye aliyempigia simu, Rais aliomba
kuongea na yeyote aliyekuwa karibu ndipo mkuu wa mkoa akampa mmoja wa
waliokuwa katika mkutano huo kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment