LIMEZUKA
wimbi jipya la vitendo vya kutisha vya kihalifu jijini Dar es Salaam,
ambavyo wahalifu wanapora watu mali na kuwajeruhi kwa silaha.
Jambo
la kushangaza ni kwamba makundi ya wahalifu yanapora watu na kuwajeruhi
kwa kutumia silaha hadharani, hali inayoonyesha kuwa vyombo vyetu vya
usalama havifanyi kazi ipasavyo.
Tunasema hivyo kwa kuwa uporaji wa mali za watu unafanyika hata mchana katika maeneo tofauti ya Jiji, vikiwamo vituo vya daladala ambavyo vimevamiwa na vijana wanaovuta bangi na kutumia dawa za kulevya.
Katika toleo letu la jana, tulichapisha habari kubwa kuhusu tukio la kundi la kihalifu lililoingia mitaani likiwa na silaha mbalimbali, yakiwamo mapanga, marungu na visu na kuwapora watu watano vitu mbalimbali na fedha kisha kuwajeruhi.
Uhalifu huo ulifanywa na kundi la vijana 17 wanaojiita “Black Americans” katika mitaa ya Mianzini na Mponda iliyopo Mbagala wilayani Temeke na kuwatoa damu majeruhi watano kwa kutumia silaha hizo.
Miongoni mwa waliojeruhiwa katika tukio hilo lililotokea juzi alfajiri, ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye alipata majeraha makubwa kichwani na kulazwa katika Hospitali ya Lugalo.
Tukio hilo lilitokea wakati majeruhi hao wakitoka majumbani kwao kuelekea kwenye maeneo yao ya kazi.
Tukio la kuporwa na kujeruhiwa watu hao huko Mbagala limetokea siku chache baada ya tukio ambalo mkazi mmoja wa Jiji, Salum Njwete almaarufu Scorpion kukamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumpora mali na kumtoboa macho Said Ally eneo la Buguruni.
Kuwapo kwa makundi haya ya kihalifu kunawafanya wakazi wa Dar es Salaam waishi katika hofu kubwa. Yamekuwa yanaibuka makundi tofauti ya kihalifu kwa mfano, Panya Road, Mbwa Mwitu, Komando Yosso na mengine, ambayo yote yamekuwa yakifanya uporaji na kuwajeruhi watu.
Kasi ya vitendo hivi vya kihalifu hainabudi kuvishtua vyombo vyetu vya usalama hususani Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka kukabiliana nayo kwa lengo la kuyatokomeza.
Kuna taarifa kuwa makundi mengi ya kihalifu yanayopora watu mali yako katika maeneo tofauti. Kwa Wilaya ya Ilala yanatajwa kuwa ni Majumba Sita njia panda ya Segerea, Tazara, Msimbazi Centre, ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco, Daraja la Salendar, barabara ya Ocean na Majani ya Chai, Lugoda. Kwa Wilaya ya Kinondoni ni Tanganyika Parkers kuelekea ufukwe wa bahari Kawe, Makuburi, Kinondoni Mkwajuni, kituo cha daladala cha Mwenge, Tandale kwa Mtogole, Mwananyamala A na Mwananyamala kwa Mama Zakaria, maarufu kama mahakama za simu.
Katika Wilaya ya Temeke yanatajwa kuwa ni mataa ya Chang’ombe, BP Kurasini, Temeke Maguruwe, pori la kiwanda cha Bia ambako kuna maficho ya wahalifu na Mbagala Kiburugwa ambako ni maarufu kwa mbwa mwitu. Lipo pia eneo la kati ya Mbagala Kizuiani na Zakhem.
Tunalishauri Jeshi la Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam lielekeze nguvu zake zote katika kuyasaka makundi yanayofanya uhalifu huo na wahusika wafikishwe katika mkono wa sheria. Ni matarajio yetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, atalifanya suala la kupambana na makundi ya kihalifu kuwa ajenda yake ya kila siku kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa mahali salama pa kuishi.
Mkakati wa kuyatokomeza makundi ya kihalifu tunashauri uanzie katika kudhibiti vijiwe vya wahuni katika vituo vya daladala ambavyo vimevamiwa na idadi kubwa ya wahalifu wengi wao wakiwa ni wapigadebe.

0 comments:
Post a Comment