Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli yuko Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam akiweka jiwe la msingi kwenye Majengo mapya kwa
ajili ya Malazi ya Wanafunzi.
Akihutubia Chuoni hapo, Rais amezungumzia suala baadhi ya Wanafunzi kudaiwa kukosa Mikopo.
Rais
amesema mwaka huu Serikali yake imeongeza fedha kwa ajili ya Mikopo ya
Wanafunzi na watatoa Mikopo kwa Wanafunzi wengi kuliko mwaka uliopita.
Hata
hivyo Rais alisema " Naomba nikiri kwamba hakukuwa na Coordination
nzuri. Kwanza ilipaswa Vyuo vyote vifunguliwe siku moja ili kuwe na
mawasiliano mazuri. Lakini kilichotokea sasa kuna vyuo vimefunguliwa
wakati Wanafunzi hawajui watapata Mkopo au hawatapata. Na cha
kusikitisha Vyuo vinakataa kuwafanyia 'Registration' . Jambo hilo sio
jema linasababisha usumbufu kwa Wanafunzi".
Rais ameiagiza Wizara husika, Bodi ya Mikopo na Taasisi zote zinazohusika kumaliza haraka tatizo hilo.
Home
News
Slider
Mikopo ya Elimu ya Juu; Rais Akiri hakukuwa na Usimamizi mzuri*aagiza mamlaka husika kumaliza tatizo hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment