Image
Image

Serikali izingatie maoni ya wadau Muswada wa Habari.


Baada ya Waziri Nape kuwasilisha muswada huo kwa kamati hiyo, jana ilikuwa zamu ya wadau wa habari kuanza kutoa maoni yao kwa lengo la kuuboresha muswada huo kuwa sheria rasmi ya kusimamia tasnia ya habari nchini.Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwapo kwa malalamiko ya wanataaluma ya habari na wadau wa habari nchini ambao waliilalamikia serikali ya awamu ya nne kwamba alitaka kuupitisha muswada huo kuwa sheria bila kuwapa fursa wanataaluma ya habari na wadau wa habari ya kutoa maoni yao, lengo likiwa ni kupata sheria nzuri.
Hata hivyo, busara za Spika mstaafu, Anne Makinda na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ya Bunge la 10, zilisaidia sana kutokana na kuielekeza serikali kuuahirisha ili wadau wapate muda wa kutosha wa kutoa maoni yao.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo jana, Nape alisema muswada huo utasaidia kuifanya sekta ya habari iwe na taaluma kamili ambayo itawezesha mfumo mzuri wa usimamizi wa tasnia hiyo. Pia alisema muswada huo umeandaliwa ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika tasnia ya habari nchini, baadhi ni upungufu wa sheria zinazosimamia tasnia hiyo.
Waziri Nape aliwataka wanahabari na wadau wa tasnia hiyo kuendelea kutoa maoni yao kabla ya muswada huo kwa ajili ya kuuboresha kabla ya kupelekwa bungeni kupitishwa kuwa sheria rasmi.
Jambo la msingi ni kwa wanataaluma ya habari na wadau wa habari kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ili muswada huo uboreshwe na kuzingatia maslahi yao, kubwa likiwa ni kulinda uhuru wa habari nchini.
Kadhalika, wanahabari na wadau hawanabudi kuhakikisha kwamba wanatumia muda wa kutosha kuupitia muswada huo ili kuelewa maudhui yake ili maoni yao yalenge kuboresha baadhi ya vifungu ambavyo watabaini kuwa na mapungufu.
Kufanya hivyo kutasaidia kuepukana na malalamiko baada ya muswada huo kupitishwa na Bunge na kuwa sheria rasmi. Ushauri wa mjumbe wa kamati hiyo ya Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, aliyewashauri wanahabari na wadau kuusoma kwa makini ili wasilalamike baada ya kupitishwa ni wa msingi na unapaswa kufanyiwa kazi.
Tunasema hivyo, kwa kuwa Watanzania wengi wana utamaduni wa kutojitokeza kutoa maoni, lakini wanakuwa wepesi wa kulalamika baada ya uamuzi kufanyika.
Tunawahimiza kufanya hivyo kwa kuwa umebakia muda mfupi ikitiliwa maanani kuwa muswada huo utawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge mwezi ujao.
Kwa kuwa wadau walishaanza kutoa maoni yao kupitia vyama vyao kabla ya mkutano wao na wabunge wa kamati jana, ni matumaini yetu kwamba serikali itayazingatia kabla ya kuuwasilisha bungeni.
Kwa kufanya hivyo, serikali itadhihirisha kwa vitendo kuwa ni sikivu na ina nia ya dhati ya kutunga sheria nzuri ya kusimamia sekta ya habari nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment