Image
Image

Shughuli ya uhamishaji wa wakimbizi nchini Ufaransa yakamilika

Shughuli ya uhamishaji wa wakimbizi kutoka kwenye kambi ya Calais nchini Ufaransa imekamilika baada ya siku tatu.
Viongozi wa utawala nchini Ufaransa wametoa maelezo na kuarifu kuhamishwa kwa wakimbizi wote kutoka kwenye kambi ya Calais.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba muda uliotumika kuondoa wakimbizi kwenye kambi ya Calais umekuwa mfupi zaidi tofauti na ilivyotarajiwa.
Viongozi hao pia wametangaza kambi hiyo kuwa itabomolewa katika siku zijazo.
Hata hivyo kulizuka ghasia wakati wa shughuli ya uhamishaji.
Baadhi ya wakimbizi waliopinga shughuli hiyo walichoma moto mahema waliyojengewa.
Kabla ya shughuli ya uhamishaji, kambi hiyo ilikuwa ikitoa hifadhi kwa wakimbizi zaidi ya elfu 8.
Wengi wa wakimbizi hao ni raia wa Sudan wapatao elfu 2 waliokuwa wakijaribu kuingia mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa kupitia Italia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment