Image
Image

Matokeo ya uchaguzi wa rais Bulgaria

Bulgaria kuendelea na duru ya pili ya uchaguzi baada ya wagombea urais kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50Nchi ya Bulgaria italazimika kufanya duru ya pili ya uchaguzi baada ya wagombea urais kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo uliyofanyika hapo jana, chama kikuu cha upinzani kinachoongozwa na jenerali mstaafu Rumen Radev kiliongoza kwa kupata asilimia 24.8 ya kura.
Chama cha GERB kinachoongozwa na waziri mkuu Boyko Borisov na mwenyekiti wa bunge Tzetska Tzacheva, kilifuatia katika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 23.5.
Hapo awali, waziri mkuu Borisov aliwahi kutangaza kwamba atajizulu endapo chama chake kitashindwa kuongoza kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.
Borisov aliitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kufuatia matokeo hayo.
Kwa mujibu wa takwimu za tume ya uchaguzi, asilimia 45.3 pekee ya wananchi ndiyo iliyoshiriki kwenye uchaguzi huo wa kumbainisha rais wa awamu ya 5 nchini Bulgaria.
Takriban raia elfu 40 wa Bulgaria wanaoishi katika nchi 71 za kimataifa pia walishiriki kwenye zoezi la upigaji kura.
Duru ya pili ya uchaguzi huo itafanyika tarehe 13 Novemba siku ya Jumapili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment