Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Baadhi
ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wametoa maoni juu ya
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ili kuuboresha na kuhakikisha
unaleta manufaa kwa waandishi wa habari, vyombo vya habari pamoja na
wananchi wa kawaida.
Maoni hayo yametolewa na wakuu hao wakati
wakihojiwa na mwandishi wa habari hii katika nyakati tofauti ambapo
wengi wameonekana kutoa mawazo chanya yenye kuboresha muswada huo.
Akiongea
na mwandishi wa habari hii, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla amesema kuwa
sheria hiyo inatoa mwanya mkubwa kwa kada hiyo kuwa taaluma
inayoheshimika kama zingine kwa sababu baada ya Muswada huo kuwa sheria,
kada hiyo itakuwa na chombo kitakachowasimamia wanahabari.
“Uanzishwaji
wa Baraza huru la Habari ambalo ni moja ya kitu kilichoainishwa na Sera
ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 iliyoitaka Serikali kuanzisha
chombo huru kitakachosimamia masuala ya habari hivyo, Muswada huu
utakapokuwa Sheria utakuwa umetekeleza agizo la Serikali la kuanzisha
chombo huru kitakachosimamia masuala hayo”, alisema Msalla.
Ameongeza
kuwa sheria hii italeta uhuru wa vyombo vya habari kwani kwa sasa
mmiliki asiporidhishwa na maamuzi ya kutopewa leseni anakata rufaa
inayoishia kwa waziri mwenye dhamana lakini baadae mmiliki wa chombo cha
habari asiporidhishwa na maamuzi ya Mhe.waziri ana uwezo wa kwenda
mahakamani.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkoa wa
Morogoro, Andrew Chimesela amekubaliana na uamuzi wa kuundwa kwa Bodi ya
Ithibati kwa sababu bodi hiyo itakua katikati kuangalia maslahi ya wana
tasnia pamoja na kudhibiti nidhamu na maadili yanayokwenda sambamba na
tasnia hiyo ili kusiwepo na dharau kwa tasnia hiyo.
Kwa upande wake
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti,
Englibert Kayombo ameunga mkono uanzishwaji wa Bodi ya Ithibati kwa
sababu itasaidia kutambua wanahabari wenye taaluma halisi katika tasnia
ya habari.
“Binafsi naunga mkono jitihada zinazofanywa na wizara
kurasimisha tasnia hii ya habari ili iwe na hadhi sawa na tasnia zingine
hivyo ni vyema kusimamia kazi za waandishi wa habari na kuwaongoza
wanahabari katika kutoa habari zenye mtazamo chanya utakaojenga taifa
letu”, alisema Kayombo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Luhende Singu amesema
kuwa sheria hiyo itavifanya vyombo vya habari kuajiri watu wenye
taaluma ya habari tofauti na ilivyo sasa pia wananchi watarajie kupata
habari za ukweli na uhakika.
Home
News
Slider
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini watoa maoni juu ya muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment