Rais Magufuli amteua Dkt. Khatib Kazungu kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Desemba, 2016 amemteua Dkt. Khatib M. Kazungu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Khatib M. Kazungu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Doto James ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Khatib M. Kazungu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Desemba, 2016
0 comments:
Post a Comment