Rais wa Ufaransa François Hollande anatamatisha Jumanne hii ziara ya kikazi nchini Colombia kwa kukutana kwa mazungumzo na waasi FARC. François Hollande atazuru eneo wanakokusanywa wapiganaji hao katika hali ya kurejeshwa katika maisha ya kiraia karibu na mji wa Cali, katika jimbo la Cauca.
Ataongozana na mwenzake wa Colombia Juan Manuel Santos.
Ziara ya rais wa Ufaransa katika eneo wanakokusanywa wapiganaji wa FARC katika hali ya kurejeshwa katika maisha ni ishara kubwa na tukio hili limechapishwa kwenye magazeti mengi nchini Colombia.
Kwa ziara hii rais wa Ufaransa anakuja kuunga mkono mchakato wa amani nchini Colombia, baada ya serikali na waasi kusaini mkataba wa amani mwaka jana.
Katika kuamua kukutana na viongozi wa waasi wa FARC, ikiwa ni pamoja na Pablo Catatumbo, Rais wa Ufaransa pia amewapa matumaini waasi, kwa kuwatambua kama wahusika wakuu katika utekelezaji wa mchakato wa amani, kwa sababu kwa sasa, waasi hao bado hawajaanza kusalimisha silaha zao.
Kundi la waasi la FARC pia limekaribisha ziara ya François Hollande, hasa kwa vile ni kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana nao wakiwa nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment