Riyad Mahrez aliokoa Algeria kuepuka kichapo toka kwa Zimbabwe na kufanya matokeo kuwa sare ya 2-2 katika mchezo uliochezwa jana wa michuano ya Kombe la Afrika (AFCON) nchini Gabon.
Mchezaji huyu bora wa Afrika mwaka 2016 aliifunga mabao 2 katika mechi hii ya ufunguzi ya kundi B uwanjani Franceville.
Alifungua kurasa wa mabao dakika ya 12. Hata hivyo, Zimbabwe ilisawazisha kupitia Kudakwashe Mahachi dakika 5 baadaye kabla ya kuchukua uongozi kupitia penalti ya Nyasha Mushekwi dakika ya 29. Mahrez alisawazishia Algeria katika dakika ya 82 baada ya kuvuta shuti kali kutoka nje ya kisanduku. Hadi mwisho wa mechi timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 2-2.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi C ambapo Ivory Coast itakutana na Togo, wakati DRC itakapomenyana na Morocco.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment