Picha kwa hisani ya Maktaba.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 2.4 kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji katika mji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Polisi Makambako mkoani Njombe Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi za salama katika umbali usiozidi mita 400 kama inavyosema sera ya maji.
Aidha amewataka wananchi kutofanya shughuli za kijamii katika vyanzo vya maji ili kuvilinda na kusisitiza Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta maji kwa sababu vyanzo vingi zimekauka kutokana na shughuli za kibinadamu.
Awali akizungumzia madai ya Fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha ukaguzi cha pamoja na soko la kitamaifa katika eneo la Makambako amesema sewrikali itawalipa fidia.
Nae Mbunge wa jimbo la Njombe Mheshimiwa SANGA amesema moja ya changamoto inayowakabili wakazi wa mji wa Makambako ni ucheleweshwaji wa malipo ya fidia kwa waliopisha ujenzi wa kituo hicho hali inayosababisha baadhi yao kwenda kudai fidia hiyo kwa kiongozi huyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment