Msani wa Hip hop nchini
Tanzania Stereo a.k.a Singa Singa ambaye ni moja kati ya Rappers waliopiga
hatua kubwa tu katika Musiki wa Hip hop ambao huwa unaonekana mgumu kwa
waliowengi na kujikuta katika eneo hilo wakiwa wachache sana wengine
wakikimbilia nyimbo laini zakuimba siku za hivi karibuni amefunguka kupitia
vyombo vya habari kuelezea hisia zake za kimapenzi kwa mtu anaye mpenda.
Stereo kupitia Radio,
Luninga(Tv) na Mitandao ya kijamii ameonekana kuwa mwenye kiu ya kufikisha
ujumbe wake kwa mtu anaye mzimia ambaye ni Chemical ambaye jina lake halisi ni
Claudia Lubao msanii mwenzie ili lau nayeye atambue kuwa anampenda na ndio
Maana ameweka hadharani, yapo mashairi ya wimbo wa Fresh Jumbe yanayosema
Mapenzi ni kikohozi kuyaficha siyawezi.
“Naweza kusema nampenda sijui
nani labda Stosh, Rosa Lee lakini nampenda
Chemical namzimia kiukweli Chemical na hata ukiniuliza kwanini sidhani
kama naweza kusema. Kila mtu anajua kinachomvutia kwa mtu anayempenda na naomba
tu nimwambie hapa Chemical, I Love You, I Feel You Chemical” – Stereo.
Stereo najua wanaume tunakuwa
tunapofikia hatua ya kumuhitaji msichana ambaye umehisi kwamba huenda akikubali
kusikia hisia zangu bhac naweza ishi naye, najua Broo ushaa fika speed zaidi ya
80 lakini Chemical bado hajafika Speed ile bado yupo chini mno katika Speed
yake.
1.Chemical anatafakari sababu
za wewe kuweka hisia zako dhidi yake mbele ya umati wa watanzania na jamii
inayo mzunguka.
2.Anatafakari kuwa una dhati
ya moyo katika unacho kisema kwakuwa hamkuwahi kuwa karibu,kwa maana sikana
kwamba wewe ni wakwanza kumtamkia kuwa unampenda wapo wanaoonesha hisia ila
wewe umeonesha kupitia Media.
3.Chemical anawaza endapo
akikubali wewe na yeye muwe wapenzi Je itakuwa nidhati ya mtima wake ama
shinikizo la Media ambazo zinapiga kelele kwamba kwanini asikukubalie kwakuwa
umeweka wazi.
4.Anatafakari familia yake
itamtizama vipi,sikana kwamba sio msichana
wakuhitaji kuwa na mtu ama
kupendwa la hasha bali nikwaujumbe uliomzito ambaon unafanya mapenzi kuwa
Spesho kwa kuwa ni siri sasa imekuwa wazi hivyo hawatostuka kuona ama kusikia.
5.Chemical anawaza kwanini
hakuweza kuomba namba akanitafuta akaweka hisia zake angali unampenda tena si
kwa sababu ya mapenzi tu bali kwa sababu ya kuja kuishi naye kama mke na mume.
6.Ikiwa kama inavyoelezwa
kuwa bado anausichana wake ama(Bikira) hudhani anaweza kuona nikigezo cha wewe
kumfuata kisha ukimaliza haja zako bhac tena.
Anachokipenda Mwanamke.
Mwanamke yapo mambo anayo
yapenda kama wewe unavyo mpenda na ulivyovipenda kwake.
1.Moja Mwanamke yeyote yule
mwenye kujitambua na nini anataka anapata furaha na raha moyoni mwake pale
unapo pata nafasi ya kuonana naye na kuzungumza kwa kinywa chako kile
unachokusudia, huwa inamjengea kumbukumbu kubwa mno kwatika mahusiano.
2.Inampa kwanza muda wa
kujitathmini kwa unachotaka kwake na dhamira yakutaka umpatie mda kama
mwanamume kusudi aweze kukutafakari kwa uzuri ili ashauriane na halmashauri
yake ya kichwa kwamba je unafaa kuwa mume ama unahitaji kuwa naye tu inatosha,
hivyo yafaa utambue hilo kuwa watu hawa wapo hivyo.
3.Mwanamke anapenda aone
dhamira ya moyo wako ukiwa unamuhitaji ili uwe naye kwa kila hatua iwe mchana
ama usiku, na maanisha nini usimtume rafiki yako akuunganishie kila kitu kwa
mtu unayemuhitaji halafu wewe uje umalizie tu kufunga goli hapana anataka iwe
mvua inayesha upo, iwe jua linawaka upo so anapokuwa rafiki yako kwa muda
ataanza kuwaza mengi hivyo jambo la kuzingatia mnoo.
4.Wanawake nao wana vitu vyao
wanavipenda ama wanatamani kuona haswa kwa mtu ambaye anahitaji kuwa naye ama
mwenye dhamira na ndio maana wanapata faraja unapo mtamkia kuwa unampenda kwa
kinywa chako unampa muda wa kukuchambua.
5.Hakuna kitu kirahisi
wanawake nao wana vipimo vyao kama tulivyo navyo wanaume huwezi jua unaweza
kuwa mtanashati lakini ukawa na vitabia visivyompendezea kama mtarajiwa wako
vikakukosesha maksi katika eneo hilo hivyo vipo vya kuzingatiwa sana eneo hilo
na ndio maana wengine hukaa hata zaidi ya miaka miwili wakichunguzana ili
kusudi iwe afadhali kiasi kwakuwa huwezi kupata iliyo 100% la hasha lakini lau
hata 85% au 95% unajua mengine yataenda sawa.
Ushauri.
Srereio Punguza Speed uliyo
nayo ipo juu mnoo, dhamira ya moyo wako ni kumuhitaji huyu mwana dada Chemical,
jipange tafuta namba yake kama huna kama unayo mjenge kifikra kwamba kama sileo
basi kesho.
Muoneshe kwamba utampenda tu
hatakama yeye hatakupenda, kwani naamini Chemical sikana kwamba kama msichana
akawa hana hisia za kupenda no na nikiangalia upande mwingine pia ni msomi wa chuo
tangu asome chuo naamini kapitia vihunzi vingi lakini kama nikuvishinda amekuwa
jasiri kwa wakati huo.
Stereo Naandika haya wewe ni
Mwanamume mwenzangu umeonyesha hisia, najua huyu Chemical siyeye tu katika hii
dunia hapana lakini mshale wa saa sasa umegota pale unapo pataka, tafuta eneo
tulivu lenye upepo unao vuma kutoka pande zote za dunia,Kaa na binti zungumza
naye tena siku hiyo nakushauri usigusie lolote kuhusu hisia zako kwakuwa huenda
akija atakuwa anawazo lile la kwamba wewe ulisha uhabarisha uma wawatanzania
kuwa unamuhitaji sasa wewe ugeuze mshale.
1.Tumia muda huo wa wewe na
yeye kukaa eneo lenye kumfanya asiwe muoga ama asiwe nashaka yakana kwamba
unaweza fanya lolote hata kwa ushawishi fulani lahasha lakini kaa naye na
uhakikisha kwamba unahitaji kupunga naye upepo tu wa bahari na kubadilishana
mawazo hata music wenu.
2.Usimbane endapo kama
akikubali kupata juice na wewe Chemical basi endapo kwa siku hiyo atahitaji
kuligusia suala la wewe kuonesha hisia kwake bhac usikatae wito kumsikiliza ila
nashauri usije ukatumia nafasi kumjibu kwa uharaka siku hiyo ukaharibu kwa
kuona ulichokuwa unakitaraji Bhac kama kinaanza kuleta matumaini.
3.Usije msogelea kwa kujaribu
kumshika ama kumgusa kwa kuonesha ishara yeyote ya uharaka wa mapenzi, lakini
zingatia una uso wa bashasha wenye kufurahia kuitikia wito wako wa kufika eneo
flani kupata juice nawe.
4.Ukipata muda onesha dhamira
ya kutengeneza urafiki wa ukaribu sasa baada ya pale naamini sasa ndipo
patakupa picha ya safari yako unayotaka kuanzisha na Chemical.
5.Usijutie kuupoteza muda
wakati unataka kutengeneza kitu kizuri kuwa mvumilivu kwa kuwa unachotaka
kukifanya si kwa sababu yetu mashabiki bali wewe na huyo unayemuhitaji ili
kusudi ifikie hatua kuona ulitumia muda lakini umepata kitu chema.
0 comments:
Post a Comment