Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika kutoka nchini Marekani kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization Procedure) kwa mgonjwa na kuzibua mshipa wa Moyo uliokuwa imeziba kwa zaidi ya miezi mitatu (kwa lugha ya kitaalamu Chronic Total Occlusion).
Upasuaji huo ambao unatumia mishipa ya damu ulichukuwa muda wa saa moja kwa kuzibua mshipa mmoja wa damu ambao ulikuwa umeziba kwa asilimia 100 na kushindwa kupeleka damu upande wa kushoto wa moyo.
Kambi ya Madakari wa Afrika imeanza tarehe 23/1/2017 na inatarajiwa kumalizika tarehe 29/1/2017. Hadi sasa jumla ya wagonjwa sita wameshapatiwa huduma za matibabu ya moyo ambayo ni kuzibua mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba. Hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na wanatarajiwa kuruhusiwa siku yoyote kuanzia kesho.
Tangu kuanza kwa mwaka huu wagonjwa 29 wameshafanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya wagonjwa hao 23 wamefanyiwa upasuaji katika kambi za ndani na wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya Madaktari Afrika.
Taasisi inaendelea kuwaomba Madaktari wote nchini wenye wagonjwa wao wa matatizo ya moyo wawatume wagonjwa hao katika Taasisi ya Moyo ili waweze kupatiwa matibabu. Kwa mawasiliano zaidi wawasiliane na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na 022-2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.
Home
Afya
Slider
Taasisi ya moyo yafanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo iliyoziba kwa asilimia 100 .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment