Baada ya kesi, Viongozi wa Chama pamoja na Wanasheria watazungumza na waandishi wa habari hapa hapa mahakamani kuhusu tukio la jana la Mwenyekiti kushikiliwa polisi hadi saa 7 usiku alipoachiliwa kwa dhamana baada ya kupekuliwa nyumbani kwake na kutakiwa kuripoti tena Jumatano wiki hii.
Aidha watazungumza kuhusu kesi hii ya kikatiba namba 1 ya 2017.
NB; Tunaomba mpuuze uzushi unaoenezwa kwa njia mbalimbali kwamba Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward atazungumza na vyombo vya habari leo, Ni habari za uongo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) tarehe 10 February 2017 alifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.
Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).
Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.
Home
News
Slider
Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura, imeshaanza Mahakama Kuu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment