Shirika la misaada linalowahudumia watoto la Save The Chilren limetoa taarifa kwamba maelfu ya watu nchini Somalia wanalazimika kuyaacha makazi yao kwa ajili ya kwenda kutafuta maji na maeneo ya mifugo yao kutokana na hali mbaya ya ukame iliyopo nchini humo.
Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Somalia, Hassan Noor Saadi amesema kwamba hali ni mbaya mno na katika maeneo mengine kinachoonekana ni mifugo iliyokufa kama ngamia jambo ambalo linasababisha simanzi kubwa kwa wamiliki wa wanyama hao. Umoja wa mataifa ulitoa tahadhari mapema mwezi huu kuwa zaidi ya watu milioni 6 nchini Somalia wanakabiliwa na janga la njaa.
Shirika hilo la Save The Children limeripoti juu ya zaidi ya watoto 360,000 walio chini ya umri wa miaka mitano ambao wanakabilibiwa na hali mbaya ya utapiamlo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa, Somalia inakabiliwa na ukame mbaya ambao umesababisha mimea kukauka huku idadi kubwa ya mifugo wakiendelea kufa.
Home
Kimataifa
Slider
Shirika la Save The Chilren lasema maelfu ya watu Somalia wanakabiliwa na Ukame.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment