Image
Image

Siku ya RADIO:Ifahamu misingi ya utangazaji kama mwana habari.

Kutoka kwa Dotto Bulendu
Kila 13 February dunia inafanya kumbukumbu ya siku ya redio duniani,Tanzania tunatajwa kuwa na redio karibu 127 zenye leseni leseni tofauti.
1.State media-Radio ya Serikali,sijui kama ipo
2.Public Media-Radio za umma hapa zipo TBC Taifa na TBC Gm
3.Commercial Radio- Mf Radio one,Radio Free Africa
4.Community Radio-Mf Radio Sengerema
5.Institutinal Radio,hizi zaweza kuwa za taasisi za kidini(Religious radio)mf Radio Maria,Radio Wapo.
6. Entertainment radio,hizi kazi yake ni kiburudisha
Kwa Tanzania Radio zinafanya kazi chininya TCRA,kila radio ina sera yake kulingana na leseni yake,ndiyo maana TBC haitakuja fanana na Clouds,wala Radio Maria haitakuja fanana na Radio Iman.
Misingi ya kale ya kazi za radio ni
1.Kuburudisha
2.Kufahamisha
3.Kuelimisha.
Leo Radio haziishii kwenye misingi hiyo ya kale Redio leo zina kazi za
1.Kuburudisha
2.Kufahamisha
3.Kuelimisha
4.Kukosoa(critic not criticism)
5.Kutafsiri
6.Kuonesha
7.Kuwasemea watu hususani makundi maalum.
Uwekezaji katika redio umekuwa unaongezeka kila kukicha nchini Tanzania,redio zinapambana kugombania wasikilizaji,huku kukiwa na kilio cha wakongwe kuwa kumekuwa na udhaifu katika ubora wa uandaaji wa vipindi na hata utangazaji!.
Watangazaji wa leo wanalaumiwa kuwa na makosa ambayo yangeepukika,mf
1.Watangazaji wengi wanaingia kwenye vipindi bila kujiandaa,wanamakosa mengi ya matamshi,mf Rna L,S na Th,Z na Dh.
2.Baadhi ya watangazaji wa leo kwenye baadhi ya redio wamekuwa wakiingia kwenye vipindi bila utafiti wala maandalizi,vipindi vingi havina takwimu,havina rejea,havina vyanzo sahihi.
3.Watangazaji baadhi wamekuwa hawazingatii misingi ya maadili ya utangazaji (broadcasting ethics)na maadili ya jamii(social ethics),kuna vipindi vimekuwa vikihamasisha maovu,lugha zinazotumika siyo za staha,mada zinazojadiliwa kuwa na ukakasi!.
4.Mvuto wa utangazaji kwa baadhi yetu unakosekana kama mvuto waliokuwa nao akina Othman Miraji,Edda Sanga,Abdul Ngarawa,Ben Kiko,Abuu Liongo,Erick Nampesya,Julius Nyaisanga,Abdul Mtulia,Suzan Mungi,Deo Kiduduye,Fred Mosha,Mikidadi Mahmoud ,Swedy Mwinyi,Juma Nkamia,n.k
Walikuwa na mvuto wa namna ya kuzichezea sauti zao kulingana na aina ya vipindi walivyokuwa wakifanya enzi hizo!
5.Baadhi ya watangazaji wamekosa ubinifu hasa linapokuja suala la aina ya utangazaji,zipo lawama kuwa watangazaji wengi wanaigana namna ya kutangaza na hata namna ya kuichezea sauti.
6.Kumekuwa na changamoto ya kujua mahitaji ya wasikilizaji(wasikilizaji wanataka nini?
7.Watangazaji leo tunabeba lawana za kutokuwa wabobezi wa lugha hususani kiswahili.
Ila pamja na changamoto hizo,Redio nyingi Tanzania zimekuwa na mwendo mzuri.
1.Kumekuwa na kazi nzuri ya ubunifu,redio nyingi zinatoka na kuwafuata wasikilizaji wake,hazijigungii kama ilivyokuwa zamani.
2.Ushirikishwaji wa wasikilizaji kwenye vipindi vya redio nyingi umeongezeka,wasikilizaji sasa wamekuwa sehemu ya maudhui ya vipindi.
3.Ubunifu katika uandaaji wa vipindi umekuwa mkubwa,vionjo kama Teaser,voxpop,music,sound effects vimekuwa ni sehemu ya vitu vinavyozingatiwa kwenye vipindi vya habari!
4.Watangazaji wa redio wengi wamemudu changamoto ya mitandao ya kijamii!
Je katika kumbukumbu hii ya siku ya redio duniani,tathmini yako ni ipi juu ya ufanisi wa redio nchini Tanzania?
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment