Akizungumza kwa simu na rais wa Jamhuri ya umma wa China, Xi Jinping, rais Trump anasemekana amehakikisha ataheshimu sera ya China moja.
Serikali ya mjini Beijing inaiangalia Taiwan kuwa ni sehemu ya ardhi yake.
Duru za ikulu ya Marekani zinasema viongozi hao wawili wamealikana kila mmoja kuitembelea nchi ya mwenzake. Mazungumzo hayo yalikuwa ya kwanza kufanyika kati ya viongozi hao wawili tangu Donald Trump alipoapishwa kuwa rais wa Marekani, Januari 20 mwaka huu.
Baada ya kushinda uchaguzi wa rais Trump aliwakasirisha viongozi wa China, aliposema amepokea risala ya pongezi kutoka kwa rais wa Taiwan na kuongeza kusema kwamba suala la Taiwan linaweza kufumbuliwa.
Matamshi hayo yaliikera China na yalionyesha kwenda kinyume na mwongozo uliokuwa ukifuatwa kwa miongo kadhaa na serikali mjini Washington.
0 comments:
Post a Comment