Wabunge nchini Uingereza wamekubali serikali ya nchi hiyo kuanza mjadala, kuzungumzia, kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Waliupigia kura kwa wingi mswada huo wa nchi kujitoa.
Muswada huo umeidhinishwa kwa kupigiwa kura na Wabunge 494, huku wengine 122 wakukataa kuupigia kura, kuweza kuiruhusu serikali ya Uingereza kuanza miaka miwili ya majadiliano ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Lakini hata hivyo, uamuzi huo sasa itapelekwa katika Bunge la juu la Uingereza (House of Lords) kwa ajili ya kutolea maamuzi ya mwisho.
Waziri Mkuu Theresa May amesema anataka kuanza mazungumzo rasmi ifikapo mwishoni mwa mwezi wa tatu.
Miongoni mwa watu waliokuwa wakiupigia kampeni Iain Duncan Smith anasema wabunge wameheshimu maoni ya wapiga kura.
Lakini kwa upande wake, Kiongozi wa Chama cha Liberal Democrat, Tim Farron alipiga kura kupinga mswada huo na anataka bado kura ya maoni katika hatua hiyo ya mwisho.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment