Image
Image

Wabunge wa Upinzani watoka nje ya Bunge kupinga kukamatwa LIssu.

Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge kupinga kukamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)  Tundu Lissu.
Wabunge hao wametoka nje ya Bunge hivi punde baada ya Naibu Spika kumtaka Mbunge wa Serengeti kutoka nje baada ya kutokea mabishano yaliyotokana na hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) ya kutaka Bunge lijadili swala Haki na Madaraka ya Bunge kukiukwa kwa wabunge kukamatwa ndani ya viwanja vya Bunge kinyume na utaratibu.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amewatoa nje ya Bunge, wabunge watatu wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda) na Marwa Ryoba (Serengeti).
Pamoja na hilo, baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi, Tundu Lissu amerejeshwa mahabusu hadi leo ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment