Image
Image

Mahakama yapinga zuio jipya la uhamiaji la Trump

Mahakama kuu ya jimbo la Hawaii nchini Marekani imeweka pingamizi la muda la nchi nzima juu ya amri iliyopitiwa upya ya Rais Donald Trump juu ya kuzuia uhamiaji nchini humo. Mpango huo ulilenga raia kutoka mataifa 6 yenye waumini wengi zaidi wa dini ya Kiislamu.
Jana Jumatano jaji wa mahakama hiyo alisema kuwa amri hiyo ya Rais Trump inakiuka katiba ya Marekani kwa kiasi kikubwa ambayo inaruhusu uhuru wa kuabudu na haki nyingine.
Rais Trump alisaini agizo hilo mapema mwezi huu akilenga kuzuiwa kuingia kwa raia wa nchi hizo 6 ndani ya kipindi cha siku 90. Agizo hilo pia lilitoa zuio la kuingia wakimbizi kutoka nchi yoyote ndani ya kipindi cha siku 120. Agizo hilo limekuja baada ya agizo kama hilo mwezi Januari ambalo lilipingwa na mahakama nyingine.
Agizo hilo lililopitiwa upya lililichochea jimbo la Hawaii kufungua mashitaka. Jimbo hilo limesema kuwa agizo hilo linakiuka katiba na "Hakuna zaidi ya zuio la pili la Waislamu". Imesema kuwa kutekelezwa kwa hatua hiyo kutaleta athari kwa kutopewa kipaumbele kwa dini hiyo.
Uamuzi huo unatarajiwa kuwa pigo kubwa kwa Trump. Jana Jumatano aliita kuwa "Uamuzi wa kimahakama uliopita kiasi ambao haujawahi kutokea".
Katika hotuba kwenye jimbo la kusini la Tennessee aliita uamuzi huo ni wa "Hovyo" na akaapa kupambana nao mpaka katika mahakama ya rufaa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment