Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Mh.Tundu Lissu amekamatwa na polisi leo akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma.
KAULI YA WAKILI KIBATALA:
Lissu hajaruka dhamana. Polisi Kanda Maalum Dar walimwambia Wakili Nashon Nkhungu aliyemdhamini Lissu na aliyekwenda kutoa udhuru Jumatatu ya tarehe 13 Machi, 2017 kwamba Lissu arudi leo tarehe 16 Machi 2017 kuripoti.
Leo Wakili Nkhungu amefika na akatoa taarifa kwa mandishi kwamba Lissu yuko Dodoma kwa kesi nyingine iliyofunguliwa na Godfrey Wasonga dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwamba kuna amri ya Jaji kwamba pande zote zifike Mahakamani saa 4 (leo).
Lissu pia anatakiwa kuwepo Arusha kwa Mkutano Mkuu wa TLS kesho tarehe 17 Machi 2017 na uchaguzi ni Jumamosi tarehe 18 Machi 2017.
Hata kama hatakuwepo Ukumbini kwa sababu yuko kizuizini; atapigiwa kura in absentia kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi TLS. Kukamatwa kwake hakutaathiri haki zake za kuchaguliwa kama Rais wa TLS.
======
Ujumbe wa Lissu:
Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.
Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi.
Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:
Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii.
Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama??? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.
Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu. Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene. Msikubali kuyumbishwa.
Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu.
Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to, wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences.
All the best.
TLS
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment