Image
Image

Sir George Kahama aagwa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa MWANASIASA mkongwe na Waziri wa Kwanza wa Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya Uhuru, Clement George Kahama `Sir George’ (89) ameagwa leo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waliomuga hivi leo katika safari yake hiyo ya milele, ni pamoja na Marais wastaafu na mawaziri wakuu wa zamani ambao wamekuwa miongoni mwa waombolezaji walioshiriki kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mwili huo  kupelekwa kanisa katoliki la mtakatifu Petro Oysterbay kusaliwa na kisha maziko yatakayofanyika makaburu ya kinondoni hivi leo 16 March 2017.
Kahama alifariki dunia 12 March 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
FAHAMU.
Kahama alizaliwa Novemba 30, 1927 na ameacha mke na watoto 11.
Msiba wa Kahama si tu ni mzito kwa familia yake, bali pia kwa taifa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa nchi kabla na baada ya Uhuru.
Kahama ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa aliye mahiri na makini katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika kudai uhuru miaka ya 1950 hadi kujitawala mwaka 1961, na baada ya Uhuru mpaka alipostaafu utumishi wake.
Alijiunga na utumishi wa umma baada ya Mwalimu Julius Nyerere kupewa fursa na watawala wa kikoloni mwaka 1958, ya kuunda Serikali ya Madaraka wakiwa na lengo la kuhakiki uwezo wa Watanganyika kujiendeshea nchi yao wenyewe.
Wakati serikali hiyo inaundwa, ndipo Mwalimu Nyerere alipomwita Kahama kutoka Bukoba, alikokuwa akifanya kazi katika Chama cha Ushirika cha Kahawa (BCU) ili ajiunge na Baraza la Mawaziri la Serikali hiyo, akamteua kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko na mwenyewe (Nyerere) akawa Waziri Mkuu.
Baadaye ilipofika Desemba 9, 1961, Tanganyika ilitangazwa kuwa huru, na Baraza la Mawaziri lenye madaraka kamili likaundwa, Kahama akiwa Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mbali ya nyadhifa za uwaziri katika wizara mbalimbali, Kahama alipata kuteuliwa kuanzisha taasisi nyeti za kimaendeleo, zikiwa ni pamoja na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Viwanda (NDC); Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA); na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment