Image
Image

DC Majid Mwanga apokea mifuko 400 ya saruji, ampa siku tano afisa elimu kumpa ripoti ya wanafunzi.



Na.Mwandishi Wetu.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majidi Mwanga amempa siku tano afsa elimu wa Sekondari Bw. Timothy Bernard pamoja na watendaji wengine wa halmashauri ya Chalinze kutoa taarifa ya wanafunzi 87 ambao hawajaripoti katika shule walizopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa kisingizio kuwa serikali imewapangia mbali na mazingira wanayoishi.
Mh.Majidi ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani kuwa makini na utendaji wao wa kazi huku akipokea mifuko ya Cement 400 kutoka kwa wadau wa maendeleo na kuagiza mifuko hiyo kupelekwa kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa,vituo vya afya na ujenzi unaondelea wa kituo cha polisi Lugoba na kuwataka viongozi kuwa wasimamizi wa mifukohiyo. 
Mapema mkurugenzi wa halmashauli ya Chalinze Bw. Edes Lukoa amesema watendaji wote kwa sasa wanahitaji kujipima katika utendaji wa kazi kabla ya kuchukuliwa hatua huku afsa elimu Sekondari Bw.Timothy Bernard akitoa taarifa za wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni 2435 kati ya wanafunzi 2522 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na 87 mpaka sasa hawajaripoti na wengine kuanza kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwepo wazazi wao kupelekwa Mahakamani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment