Image
Image

Mkutano wa Roma na wanahabari eneo lapatikana, kueleza kadhia iliyowakumba baaada ya kutekwa.

Wakati kukionekana kuwepo Giza kwa atakapo kutana na kuzungumza na wanahabari Msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki na wenzake, kuelezea maswaibu yaliyowakuta baada ya kutekwa, Katibu mkuu wa Tuma ameeleza utakapo fanyikia mkutano huo hivi leo.
Katibu huyo wa Chama cha wanamuziki wa kizazi kipya(TUMA) Bw.Samwel Mbwana ‘Brayton’, ameeleza kuwa kilichokuwa kikichelewesha ni kuona sehemu salama ya kufanyika kwa mkutano huo, ambapo waliwaza wafanyie Tongwe records lakini wakaona si vyema sasa mkutano huo utafanyika Saa nane Mchana kwenye Ukumbi wa habari Maelezo hivi leo 10 April 2017.
Hivi leo Kaka wa Msanii Roma, Omary Musa lisema mkutano huo ungefanyika saa tano lakini hakuweka wazi eneo ambapo mkutano huo ungefanyikia kwa kile alichodai bado hawajapata eneo, jambo lililozusha hofu kwamba huenda mkutano huo haupo tena.
Bwana Musa alisema, "Bado tunatafuta kuna watu wamepewa jukumu hilo, hatuwezi kufanyia popote lazima liwe eneo salama, hatujui waliomteka walikuwa na nia gani"
"Nipigie baada ya dakika 45 nitakuwa nimeshajua, muhimu kuweni na subira tutawataarifu," amesema Musa.
Aidha Chama cha Muziki wa Kizazi kipya (TUMA) nacho kinajipanga kutoa tamko lao kuhusiana na utekwaji huo wa Roma na wenzake kwenye ukumbi huo huo wa Habari maelezo kuelezea umma kilichotokea.
Jumamosi iliyopita baada ya kupatikana akiwa kituo cha polisi Osterbay Roma aliahidi kuzungumza na waandishi leo kuelezea kilichotokea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment