Image
Image

Mmiliki wa Tongwe Records J. Murder asema bado giza alipopelekwa Roma na wenzake 3.

Baada ya taarifa za kuvamiwa kwa Roma Mkatoliki pamoja na wenzake watatu wakiwa katika studio za Tongwe Records mmiliki wa Tongwe Records J. Murder bado anaona giza nene mbele kwa kilicho tokea kwa kua haelewi mpaka sasa alipopelekwa Roma na wenzake.
Baada ya taarifa hizo kuwa gumzo mmiliki huyo wa Tongwe Records amekuwa akifanya mahojiano na Media nyingi nchini na swali kuu ni Je,wapo watu walifika studioni humo, na wameondoka na roma na wenzake? alijibu kama hivi.
"Ni kweli jana mida ya saa moja walikuja watu ambao hawajulikani wametokea wapi, wakaniulizia mimi pamoja na Roma japo mimi hawakunipata. Ikabidi wamuhoji Roma na wakaingia studio wakachua baadhi ya vitu na kuwachukua baadhi ya watu na kuondoka nao.
“Amechukuliwa Roma, Moni, Bello na kijana wa kazi wa mama yangu anaitwa Emma na hatujui wako wapi na wanahojiwa kitu gani, ila mpaka sasa napokea simu nyingi zikiwaulizia ndugu zao wako wapi, lakini mimi hadi sasa hivi sijui Roma yupo wapi.” – J. Murder.
Kusikiliza Bonyeza Play hapa chini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment