Image
Image

Rais Magufuli amteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Prof. Kitila Alexander Mkumbo anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.
Kabla ya Uteuzi huu Prof. Kitila Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt.Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt.Leonard Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
KufuatiauteuzihuoaliyekuwaKatibuMkuuwaWizarayaElimu, SayansinaTeknolojia Bi. MaimunaTarishiamehamishwanakuwaKatibuMkuuOfisiyaWaziriMkuu(Bunge).
Bi.Maimu na TarishianachukuanafasiiliyoachwanaMussaUlediambayeuteuzi wake ulitenguliwa.
Mhe.Rais Magufuli amemteua Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt. Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizarahiyo.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt.Ave Maria Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Wateule hao wataapishwa kesho tarehe 05 Aprili, 2017 saa 3:00 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Aprili, 2017
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment