Image
Image

Rais Magufuli awaapisha wajumbe 8 aliowateua kuchunguza mchanga wenye madini.

Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewaapisha wajumbe wa kamati maalum ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Hafla ya kiapo kwa wajumbe wa kamati hiyo imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mwanasheria mkuu wa serikali Mhe. George Masaju, katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa maadili jaji Harold Nsekela na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kamati hiyo ya wanasayansi wanane walioteuliwa na Mhe. Rais Magufuli tarehe 29 machi, 2017 inaongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Abdulkarim Hamis Mruma na itafanya kazi ya uchunguzi kwa siku 20 kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Mhe. Rais.
Akizungumza baada ya kuwaapisha, rais Magufuli amewataka  wawawakilishe watanzania zaidi ya milioni 50 ambao wanataka kujua ukweli kuhusu rasilimali yao ya madini.
Mhe. Dkt. Magufuli amewahakikishia kuwa serikali itatoa kila aina ya ushirikiano kufanikisha kazi hiyo na ametaka wawe huru kutumia vitendea kazi vyovyote vinavyohitajika zikiwemo maabara mbalimbali za taasisi za serikali na nyinginezo.
Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amesema baada ya kuunda kamati hiyo ya wanasayansi ataunda kamati nyingine ya wachumi na wanasheria kwa ajili ya kufanya tathmini na kuiangalia sera na sheria ya madini kwa lengo la kupata taarifa zaidi juu ya biashara ya madini hapa nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment