Mabingwa wapya Chelsea wamesheherekea ubingwa wao wa EPL ligi kuu ya Uingereza wakicheza uwanjani kwao Stamford Bridge kwa kuwatwanga Watford 4-3 katika mechi ya kukamilisha ratiba.
Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na John Terry ambaye anastaafu kucheza soka, mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Cesar Azpilicueta, Michy Batshuayi na Cesc Fabregas kukwamisha bao la 4 na la ushindi. Mechi nyingine ya ligi hiyo Arsenal imeitandika Sunserland goli 2-0 magoli yaliyofungwa na Alexis Sanchez. Nayo Manchester City imeizamisha WBA 4-1 huku Pablo Zabaleta akiaga rasmi kustaafu soka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment