Image
Image

Rais Magufuli amuweka Prof.Muhongo kwenye mtego wa kujitumbua Mwenye.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipitia moja ya Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam 24 Mei, 2017.
Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemtaka waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo kujipima na kutathmini nafasi aliyonayo katika wizara hiyo ikiwezekana aiachie kuanzia leo kutokana na kudaiwa kushindwa kuisimamia ipasavyo wizara hiyo.
 Profesa Sospeter Muhongo -  Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania 
Rais Magufuli pia ameivunja bodi ya ukaguzi wa madini TMAA na kumsimamisha kazi ofisa Mtengaji mkuu wake ambapo ameagiza dola na taasisi ya kudhibiti kupapambana na rushwa TAKUKURU kuchunguza wafaynyakazi wa bodi hiyo.
Aidha uamuzi wote huo Rais Magufuli ameuchukua baada ya kamati Maalum aliyokuwa ameiunda ikiongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma kuchunguza kiwango naaina ya madini kwenye makontena 277 ya makinikia yanayoshikiliwa bandari ya Dar es Salaam.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment