Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, 29 Mei 2017.
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya (IGP) Simon Sirro Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amemvisha IGP Simon Sirro cheo kipya, baada ya hapo Mkuu huyo mpya alikula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.
28 Mei 2017 Rais Dkt.Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Jeshi hilo Ernest Mangu na kumteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro kuwa IGP.
Katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano kwa waandishi wa Habari ilisema IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Video.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment