Taarifa iliyotolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi.John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof.Egid Beatus Mubofu umeanza tarehe 02 Mei, 2017.
Prof.Egid Beatus Mubofu (Pichani juu hapo) aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw.Joseph Masikitiko ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Bw. Joseph P. Masikitiko aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kabla ya kutenguliwa.
Gerson Msigwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Mei, 2017
0 comments:
Post a Comment