Licha ya kukabiliwa na mvua kubwa wakazi wa Mji wa Bangui walijitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Akiwa katika ziara yake ya siku nne Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa siasa Mjini Bangui na pia atautembelea Mji wa Bangassou uliopo Kusini mwa nchi hiyo eneo ambalo limeathirika zaidi na vurugu hizo.
Bwana GUTERRES pia anatarajiwa kuwatembelea waathirika wa udhalilishaji wa jinsia uliofanywa na walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.
Kabla ya ziara ya Bwana GUTERRES viongozi wa Kiislam na wa Kikristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati waliutaka Umoja wa Mataifa kuufanyia mabadiliko makubwa mfumo wake wa walinzi wa amani.
0 comments:
Post a Comment