Image
Image

Kukatika kwa umeme nchini, Waziri wa nishati aagiza vigogo 3 Tanesco kujiuzulu.

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani aagiza Naibu Mkurugenzi wa uzalishaji na Naibu Mkurugenzi wa usafirishaji Tanesco na Meneja udhibiti mitambo Tanesco, kuandika barua ya kujiuzulu endapo umeme hautarejea katika hali ya kawaida mpaka kufikia leo jioni.
Waziri Kaelemani Amelazimika kutoa kauli hiyo leo alipotembelea mitambo ya Kinyerezi na Ubungo jijini Dar es Salaam kufuatia tatizo lililojitokeza takribani siku mbili mpaka hivi leo la kukatika umeme nchini, ambapo pia ameagiza Meneja wa kituo cha kuzalisha umeme cha kidatu aondolewe leo leo katika nafasi hiyo. 
Jana Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa majira ya Saa 12:30 imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na kusababisha Mikoa hiyo kukosa umeme.
Jitihada zimefanyika ili kurejesha umeme na baadhi ya Mikoa imeshaanza kupata huduma ya umeme
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi.
TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.
Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
25/10/2017
=======
UPDATE: Oktoba 26, 2017
Tunapenda kuwataarifu Wateja wetu waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa leo Alhamisi Oktoba 26, 2017 majira ya Saa 12:03 Asubuhi imetokea hitilafu tena kwenye Gridi ya Taifa na kusabisha Mikoa hiyo kukosa umeme.
Mafundi wanafanya jitihada usiku na mchana ili kuhakikisha hali hii haijirudii na umeme unarejea katika hali ya kawaida kwa haraka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment