Rais John Pombe Magufuli amevitaka vyombo vya dola nchini kuwashungulikia watu ambao wamekuwa wakipika data za uongo za serikali na kuzichapisha sehemu mbalimbali na kusema watu hao wanapaswa kufikishwa Mahakamani.
"Niwaombe Watanzania wengi tofauti na wale wachache wanaopiga kelele muwapuuze, mtu ambaye anabadili data za serikali na kusema kuwa uchumi umeshuka nadhani wanapaswa kuchukuliwa hatua vyombo vya dola na wewe Profesa Kabudi ni Waziri wa Sheria muanze kuangalia watu wa namna hii ambao kwao kubadili Takwimu wanaona kitu kidogo, nafikiri kuna sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kunakifungu kinasema mtu anayebadilisha Takwimu za serikali anaweza kufungwa hata miaka 2 jela, kwanini hatuvitumii hivi? Unakuta mtu anazungumza makusanyo ya serikali yameshuka wakati anajua kabisa si kweli" alisema Rais Magufuli.
Amesema hayo leo katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya pongezi maaalum kwa wajumbe waliohusika kuchunguza kiwango, aina ya madini katika mchanga wa madini ambao ni makinikia.
Amesema ipo haja ya Waziri wa Sheria na vyombo vya dola kuangalia namna inavyowezekana kuwashughulikia watu ambao wanapika data.
Aidha Rais ameongeza kwa kusema kuwa mapato ya nchi hayajashuka ndiyo maana Serikali imeweza kununua ndege zaidi ya sita kwa mpigo, serikali imeweza kujenga barabara kwa fedha za ndani, na kusema serikali imeweza kujenga reli kwa kuwa uchumi wake ni mzuri.
Home
News
Slider
Rais ataka watu wanaotoa taarifa ambazo hazina ukweli kushughulikiwa na kufikishwa Mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment