Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpiga alisema jana wizara yake imejipanga kuendelea na operesheni maalum ya kukamata na kuondoa mifugo yote inayoingizwa kutoka nchi jirani kupitia mikoa ya mipakani ya Katavi, Kigoma, Tanga, Mara, Ruvuma, na Arusha na kuagiza wakuu wa mikoa na wilaya hizo kuendesha opresheni hizo maalumu ndani ya siku saba.
Ng’ombe waliouzwa Mwanga walitoka Kenya. Mpina alisema Serikali haipo tayari kuingia gharama ya kutibu magonjwa yanayoletwa na mifugo inayoingizwa nchini kinyemela na kuleta uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo, kusababisha mmomonyoko wa udongo na kuchangia kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Mpina alisema watu wenye nia mbaya wasihusishe operesheni hiyo na uhusiano ya nchi hizi mbili akitolea mfano uhusiano wa Kenya na Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yapo kisheria.
0 comments:
Post a Comment