Image
Image

Zitto Kabwe ang'aka, "Kupikwa Kwa takwimu za Pato la Taifa" Taarifa kamili ipo hapa

Taarifa yetu kuhusu ' kupikwa ' Kwa takwimu za Pato la Taifa tutaitoa mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Act Wazalendo kitakachoketi 28/10/2017. Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali. 
Tunatumia takwimu za Serikali kuonyesha kuwa Serikali inadanganya Kwa kutokusema ukweli wote wa uhalisia wa uchumi na kuporomoka Kwa mapato. 
Ni sawa na mtu anayesema Glasi ni ' half empty or half full ' kwani anasema kitu kile kile. 
Kwa mfano, Rais anaposema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa Kwa kutumia ongezeko la kodi anakuwa anadanganya Wananchi na anafanya hivyo akijua anadanganya. Rais anajua kuwa Deni la Taifa limeongezeka mno katika miaka yake miwili ya urais. ( Deni la Nje limeongezeka mpaka US$1.5bn kati ya July 2016-July 2017. Deni la ndani limeongezeka mpaka TZS 2trn katika kipindi hicho. Soma . http://www.bot.go.tz. 
Pia Rais anajua kuwa Serikali inatumia, bila kufuata sheria, Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo Benki Kuu kulipia baadhi ya Miradi yake. Kukiuka sheria za Fedha ni kosa la jinai na wakati mwengine kosa la kikatiba kwani Katiba imeweka utaratibu wa masuala ya Fedha za Umma. 
Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu. Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi Kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma. Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA
Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama
Act Wazalendo
24/10/2017
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment